Mei, 2008 
|
| S |
M |
T |
W |
T |
F |
S |
| | | | | 1 | 2 | 3 |
| 4 | 5 | 6 | 7 | 8 | 9 | 10 |
| 11 | 12 | 13 | 14 | 15 | 16 | 17 |
| 18 | 19 | 20 | 21 | 22 | 23 | 24 |
| 25 | 26 | 27 | 28 | 29 | 30 | 31 |
2008 
|
|
|
|
| |
| |
Maendeleo ya Mtandao:
Kitengo cha Huduma za Mtandao za UM,
Idara ya Habari kwa Umma, Hakimiliki © , Umoja wa Mataifa, 2006
|
|
|
|
     |
|
A’khms 08 Mei 2008
| hamishia mp3
|
 |
 |
UM inakithirisha huduma za kiutu Myanmar kufuatia Kimbunga Nargis
Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba ndege iliochukua tani 25 za metriki za vifaa vya kuhudumia mahitaji ya dharura, iliwasili Yangon, Myanmar Alkhamisi. Hii ni ndege ya kwanza ya UM kuruhusiwa kuingia nchini humo, na kufuatiwa baadaye na ndege nne nyengine, ambazo zimeshatayarishwa kupeleka misaada ziada inayohitajika kuhudumia umma ulioathirika na Kimbunga Nargis kilichopiga Myamar karibuni.
Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti wataalamu wanne wanaowakilisha timu ya UM ya Kutathminia Mahitaji Halisi ya Umma Penye Maafa Maumbile nao pia wanajianda kwa hivi sasa kuelekea Myanmar kuendeleza ukaguzi wao.
 |
|
 |
 |
Dereva wa WFP kauawa kwenye kituo bandia cha ukaguzi Usomali
Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza na kulaani vikali mauaji yaliotukia Ijumatano katika eneo la kati la Usomali, ambapo dereva aliyeajiriwa na shirika hilo alipigwa risasi na kuuawa na mwanajeshi wa mgambo wakati aliposimamishwa kwenye kituo bandia cha ukaguzi kilichopo kilomita 30 kaskazini ya Galkayo, kwenye jimbo la Mudug. WFP ilishtumu kitendo hiki ambacho ilisema ni cha pili kutukia mwaka huu na kusababisha kifo kwa watumishi wao. Ama ile shehena ya chakula ya tani za metriki 275 iliopakiwa kwenye lori husika la UM, imesalimika na haikuibiwa.
WFP iliwatumia aila ya marehemu dereva mkono wa pole na taazia. |
|
 |
 |
KM achukizwa na mashambulio ya raia vijijini Darfur
KM Ban Ki-moon ametangaza kusikitishwa sana na mashambulio ya mabomu yaliotukia karibuni katika Darfur Kaskazini, dhidi ya raia, hususan yale mashambulio yalioharibu, kwa makusudi skuli, vituo vya maji na soko kwenye vijiji vya Um Sidir, Ein Bassar na Shegeg Karo. Vitendo hivi, alihadharisha KM, kwa kupitia msemaji wake, hukiuka sheria za kimataifa na havikubaliki kamwe. Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Darfur lilisaidia kuwapeleka hospitali kwa matibabu, majeruhi wa tukio hilo vijijini.
 |
|
 |
 |
|
|
|
 |
| |
sikiliza
| hamishia mp3
| archive
|
Siku ya Kumbukumbu ya Kumaliza Biashara ya Utumwa Ulimwenguni (Sehemu ya II)
Katika makala iliopita, tulimsikiliza Mjumbe wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika UM, Balozi Augustine Mahiga akitufafanulia maana halisi ya hii Siku ya Kumbukumbu ya Kumaliza Biashara ya Utumwa Ulimwenguni, kwa wanachama wa Umoja wa Afrika.
|
|
|
|
|
 |
| |
sikiliza
| hamishia mp3
| archive
|
Tathmini ya Mjumbe wa Tanzania kuhusu kikao cha UNCTAD XII
Taasisi ya UM juu ya Masuala ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ilikutana Accra, Ghana kwenye kikao cha 12 kuzingatia matatizo ya uchumi maendeleo katika mataifa masikini yanayochochewa na utandawazi wa kihorera kwenye soko la kimataifa. Mkutano ulihudhuriwa na wajumbe karibu 4,000 waliowakilisha serikali, sekta za biashara na vile vile wawakilishi wa jumuiya za kiraia.
|
|
|
|
|
|
|